Home Habari za michezo KISA PAPE SAKHO…LUIS MIQUISSONE ATAJWA TENA SIMBA….TATIZO LAKE LAWEKWA WAZI…

KISA PAPE SAKHO…LUIS MIQUISSONE ATAJWA TENA SIMBA….TATIZO LAKE LAWEKWA WAZI…


IMEELEZWA kiungo wa Simba, Msenegali, Pape Ousmane Sakho ana uwezo wa kuipa timu ushindi kutokana na aina ya uchezaji wake wa kutumia nguvu.

Sakho amekuwa na msimu mzuri hasa mechi za mwisho ligi ikienda ukingoni na amehusika kwenye amefunga mabao sita na asisti sita, na baadhi ya nyota wa zamani wamechambua uwezo wake wakimwelezea jinsi alivyo hatari akiwa na mpira mguuni na huwa hatabiriki.

Straika wa zamani wa Yanga, Malimi Busungu anamfananisha na alichokuwa anakifanya Luis Miquissone akidai;

“Sakho akiwa na mpira mguu hatabiriki anataka kufanya nini, ni hatari, uchezaji wake naufananisha na Miquissone, tatizo amechelewa kuonyesha maufundi yake mbele ya mashabiki wake.”

Mtazamo wake uliungwa mkono na staa wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel aliyesema “Japokuwa mashabiki wamechelewa kuona ufundi wake, nilisema tangu alipofanya vizuri mechi za Kombe la Mapinduzi ni mchezaji hatari endapo akiwa na muendelezo wa kiwango chake.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA STORI ZA KUTAKA KUTEMWA....KAMBOLE KAPONA NA KUANZA MAZOEZI FASTA...DIARA KUKOSEKANA MECHI YA LEO...