Home Habari za michezo BALAAH HILI….!! GWIJI GENK AMKATAA SAMATTA HADHARANI…AFUNGUKA A-Z JINSI TIMU ITAKAVYOYUMBA…

BALAAH HILI….!! GWIJI GENK AMKATAA SAMATTA HADHARANI…AFUNGUKA A-Z JINSI TIMU ITAKAVYOYUMBA…

Habari za Michezo

Nyota wa zamani wa KRC Genk na timu ya taifa la Ubelgiji, Marc Degryse ameponda uamuzi wa timu hiyo kumuuza Paul Onuachu katika dirisha la Januari huku akidai nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta hatoshi kuziba pengo lake.

Degryse, mwenye miaka 57, alisema hayo siku chache zilizopita alipokuwa akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini humo.

“Hupaswi kudharau athari (ya kumuuza Onuachu). Alikuwa mfungaji bora. Alijihakikishia mabao 20 hadi 30 kila mwaka.

“Mashindano hayatajali kuondoka kwa Onuachu. Ndiyo, hii inaweza kuigharimu Genk kwenye mbio za ubingwa.

“Onuachu, tangu kuanza kwa 2020/21, alifunga mabao 75 katika mechi 102, mabao 17 kati ya hayo aliyafunga katika nusu ya kwanza ya msimu huu. Linganisha hilo na Samatta ambaye anapaswa kuvaa viatu vyake,” alisema nyota huyo.

“Lazima ushughulike na Samatta, kwa sababu yeye ndiyo yuko pale mbele sasa. Lakini hawezi kuwa kama Onuachu,” alisema na kuongeza: “Bado mambo yanaweza kwenda kombo kwa Genk. Kwa sababu, wakati huo huo, Union Saint-Gilloise inaonekana kuwa kwenye kiwango kizuri kwa sasa.”

Samatta alikuwa mfungaji mahiri katika muhula wake wa kwanza akiwa Genk, akifunga mabao 32 msimu wa 2018/19 pekee. Lakini baada ya uhamisho wa Pauni 10 milioni kwenda Aston Villa Januari 2020, ilitarajiwa kuwa mwanzo wa Samatta kufanya makubwa zaidi lakini imekuwa tofauti.

SOMA NA HII  FAGIA FAGIA LIGI KUU....JE YANGA KUONDOKA NA MKENYA WA TZ PRISONS..?