Home Uncategorized SIMBA; KUFUNGWA NA YANGA SIO MWISHO WA KUPAMBANA, MASHABIKI TUPENI SAPOTI

SIMBA; KUFUNGWA NA YANGA SIO MWISHO WA KUPAMBANA, MASHABIKI TUPENI SAPOTI

JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kuchapwa kwao mbele ya Yanga sio mwisho wa mapambano.

Bocco mwenye mabao matatu na pasi moja ya bao alishuhudia timu yake ikichapwa bao 1-0 na watani zao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa.

“Haina maana kwamba kufungwa kwetu ndio mwisho wa mapambano hapana kazi bado inaendelea na tuna mechi mkononi ambazo tunaamini tutapata matokeo, mashabiki wasikate tamaa nasi pia tutaendelea kupambana,” amesema.

Mchezo wa kwanza Simba ikiwa nyumbani ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2 mbele ya Yanga na mchezo wa pili ilinyooshwa kwa bao 1-0 mbele ya wapinzani wao wa jadi Yanga.

SOMA NA HII  MNAOCHIPUKIA MSIZIPE NAFASI PROPAGANDA ZA HUMUD WA MTIBWA SUGAR