Home kimataifa HUU HAPA MCHEZO ULIOWAKUTANISHA WALIOTUMIA MKWANJA MREFU ZAIDI

HUU HAPA MCHEZO ULIOWAKUTANISHA WALIOTUMIA MKWANJA MREFU ZAIDI


 HUKO Ulaya unaambiwa kuna timu ambazo zimefanya usajili ghali na kutumia mkwanja mrefu kuboresha vikosi vyao na walipokutana uwanjani ilikuwa ni mechi iliyoweka rekodi ya kuwa mechi ghali zaidi duniani.


Ilikiwa ni Septemba 28 ambapo mabosi hao walikutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa kati ya PSG inayonolewa na Kocha Mkuu, Mauricio Pochettino dhidi ya Manchester City ya Pep Guardiola. 

Dakika 90 zilimeguka kosi la PSG liliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kuwapoteza mabingwa wa Ligi Kuu England,  Manchester City. 

Kosi la PSG kwa mujibu wa Trasfermarkt data limegharimu euro milioni 997.25 sawa na trilioni 2.69 za Bongo huku kosi la City likiwa lina thamani ya Euro bilioni 1 sawa na trilioni 2.7 za Bongo.


Ikiwa utachukua thamani ya vikosi hivyo na kuijumlisha unapata kiasi cha euro bilioni 2 sawa na trilioni 5.4 kwa pesa za Bongo mkwanja ambao ni mrefu kinomanoma na unatajwa kuwa mchezo uliokuwa ghali zaidi katika ulimwengu wa soka.



City inashika rekodi ya kutumia mkwanja mrefu kumsajili mchezaji ghali zaidi kwa sasa ambaye ni Jack Grealish aliyeigharimu City euro milioni 177.5 sawa na bilioni 318 aliibuka hapo akitokea Aston Villa na alisaini dili la miaka sita.


PSG hawakuwa nyuma wana  maingizo mapya kibao yaliyoikamua mkwanja mrefu ikiwa ni pamoja na Lionel Messi mshindi wa Ballon d’Or mara sita na aliibuka hapo akitokea Barcelona. 


Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Messi aliweza kuandika rekodi yake mpya kwa kufunga bao lake la kwanza akiwa ndani ya PSG chini ya kocha Pochettino.


PSG wanatajwa na Transfermarkt kwamba ina safu ghali ya ushambuliaji ikiwa na thamani ya euro milioni 340 ambazo ni sawa na sh bilioni 920 na milioni 188.


Kumbuka kwamba safu ya ushambuliaji ina Kylian Mbappe mwenye thamani ya euro milioni 160 sawa na sh bilioni 433, Neymar Jr euro milioni 100 sawa na bilioni 270.6 na Messi euro 80 milioni sawa na bilioni 216.

SOMA NA HII  POGBA ATUPIA MABAO 28 NDANI YA MANCHESTER UNITED

Hii inamaana kwamba mpira  ni  uwekezaji na mkwanja lazima utumike ili kufikia mafanikio katika ulimwengu wa sasa ambao ushindani ni mkubwa kila sekta.