Home Habari za michezo RASMI…CHELSEA YAINGIA ZAMA MPYA….YAPATA MMILIKI BILIONEA MPYA…NI MMAREKANI…

RASMI…CHELSEA YAINGIA ZAMA MPYA….YAPATA MMILIKI BILIONEA MPYA…NI MMAREKANI…


Bilionea, Todd Boehly ameripotiwa kushinda katika kinyang’anyiro cha kuinunua Chelsea baada ya kuafiki mkataba wenye thamani ya pauni bilioni 3.5.

Kulingana na jarida la The Telegraph, Mmarekani huyo atathibitishwa kuwa mnunuzi anayependekezwa na klabu hiyo, ingawa hakujawa na uthibitisho rasmi kutoka kwa kundi la Boehly, Chelsea au Raine, benki inayosimamia mauzo hayo.

Boehly aliingia kwenye orodha fupi ya mwisho, ambayo pia ilijumuisha muungano wa Stephen Pagliuca na Sir Martin Broughton. Dau la Sir Martin Broughton lilikuwa limeungwa mkono na pauni milioni 10 kila mmoja kutoka kwa nyota wa F1 Lewis Hamilton na mchezaji wa tenisi Serena Williams.

Mr. Todd pia alikabiliwa na ushindani kutoka kwa tajiri mkubwa zaidi wa Uingereza Jim Ratcliffe, ambaye aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho saa 11 baada ya kuwasilisha ombi la £4bn.

Inasemekana Ratcliffe alikutana na mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck kujadili ununuzi huo, huku ofa yake ikizua mkanganyiko baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na wahusika wengine watatu. Lakini ofa ya Ratcliffe inaonekana kuchelewa sana kwani Todd anatazamiwa kuisaidia klabu hiyo.

SOMA NA HII  MPOLE: "SIMBA IANGALIWE KWA JICHO JINGINE...UBORA WA SIMBA UMEIFANYA YANGA KUJITAFAKARI