Home Habari za michezo KUMBE BENCHIKAH AKUMBWA NA MATATIZO HAYA MAZITO…SIMBA WANYOOSHA MIKONO JUU

KUMBE BENCHIKAH AKUMBWA NA MATATIZO HAYA MAZITO…SIMBA WANYOOSHA MIKONO JUU

Habari za Simba leo

TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba kati yetu na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha pamoja na wasaidizi wake wawili Kamal Boujnane na Farid Zemit.

Mwalimu Benchikha ameomba kuvunja mkataba wake kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili nyumbani kwao Algeria.

Mwalimu Abdelhak Benchikha ameueleza uongozi wa Simba kuwa anauguliwa na Mkewe hivyo anahitaji muda kuwa karibu nae na kumuuguza. Kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hilo Uongozi umeridhia ombi la Mwalimu Abdelhak.

Uongozi wa klabu ya Simba unamshukuru Mwalimu Abdelhak Benchikha kwa kipindi chote alichotuma ndani ya timu yetu na tunamtakia kila la heri na tunamuombea Mkewe apate afya njema.

Wakati huo huo, Uongozi wa klabu umemteua Mwalimu Juma Mgunda kukiongoza kikosi akisaidiwa na Selemani Matola hadi hapo Bodi ya Wakurugenzi itakapotoa uamuzi mwengine.

Mwalimu Juma Mgunda ataanza kazi katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi Namungo FC utakaochezwa April 30, Ruangwa Mkaoni Lindi katika Uwanja wa Majaliwa saa 12 jioni.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA UKAME WA MAGOLI UNAMZIDI...MAYELE AIBUKA NA HILI YANGA...AAMUA KUJIWEKA KANDO....