Home Habari za michezo FEI TOTO ATAJA KIKOSI BORA CHA MSIMU…AMTAJA POCOME…CHAMA NJE

FEI TOTO ATAJA KIKOSI BORA CHA MSIMU…AMTAJA POCOME…CHAMA NJE

fei toto na habari za simba leo

Kiungo wa Zamani wa Yanga anayekipiga Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto‘ ambaye amepachika mabao 19 msimu huu akisema ndio msimu wake bora licha ya kukosa mataji.

Pia ametaja kikosi chake bora cha msimu akiwajumuisha nyota 8 wa Yanga, na watatu wa Azam, ambao anaamini wakicheza mechi hakuna wa kuwazuia.

Akizungumza na Crown Media kabla ya mchezo wake wa fainali ya FA dhidi ya Yanga, Fei Toto, amesema alikuwa na msimu mzuri kuliko misimu yote aliyocheza Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kukosa mataji.

“Tangu nimeanza kucheza soka la ushindani sijawahi kufunga idadi kubwa ya mabao kama msimu huu hivyo nakiri kuwa huu ndio ulikuwa bora na wa ushindani kwangu nafurahi nimeumaliza salama,” alisema na kuongeza.

“Nimekutana na wachezaji wengi bora na wamenipa changamoto kutoka timu pinzani ni wengi wamefanya vizuri lakini kuhusu kikosi bora haya ni maoni yangu binafsi,” alisema.

Akitaja kikosi hicho, Fei Toto alisema langoni anaanza na Djigui Diarra kipa namba moja wa Yanga, Attohoula Yao, Pascal Msindo, Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Yeison Fuentes, Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Fei Toto na Joseph Guede.

“Siwezi kumuelezea mchezaji mmoja mmoja kwanini nimemtaja nafikiri namba zao zinajieleza namna walivyozisaidia timu zao na huo ni mtazamo wangu mimi,” alisema Fei toto.

Lakini aliongeza kwa kutaja wachezaji wake ambao watakuwa wa akiba, akimtaja mchezaji kama Clatous Chama, Mohammed Hussein, Maxi Nzengeli.

Fei Toto amekuwa akihusishwa zaidi kujiunga na Simba, huku yeye mwenyewe akiulizwa amekuwa akijibu yupo tayari kucheza Simba kwa moyo mmoja hivyo kama wanamuhitaji wafuate taratibu za usajili kwa Viongozi wa Azam FC.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIDHANI GSM NDIO KILA KITU...ENG HERSI AMTAJA ALIYEIPA MAFANIKIO YANGA...