Home Habari za michezo KAIZER CHIEF YAIBA KOCHA YANGA…MUDA WOWOTE KUTAMBULISHWA

KAIZER CHIEF YAIBA KOCHA YANGA…MUDA WOWOTE KUTAMBULISHWA

NASRADINNE NABI-YANGA

NASRADDINE NABI Aliyewahi Kuifundisha Yanga SC na kutwaa mataji yote ya ndani, Muda wowote anaweza kutangazwa kama kocha Mkuu wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ili kurithi mikoba ya Molefi Ntseki aliyefutwa kazi.

Nabi ambaye anakinoa kikosi cha Far Rabat amekabakiza mechi moja tu ya Ligi Kuu ya Morocco kabla ya kumaliza msimu na tayari inaelezwa amewaambia Viongozi wa klabu hiyo hatosalia kwa msimu ujao.

Nabi ana nafasi kubwa ya kutua Kaizer baada ya AmaKhosi kumhitaji tangu alivyoondoka Yanga mwishoni mwa msimu wa 2022/2023.

Dili lake la kwanza kwa AmaKhosi lilikwama kutokana na hitaji lake la kutaka kutua na benchi nzima alililokuwa nalo Yanga ndipo akaibukia Rabat.

Akiwa na miamba hiyo ya soka nchini  Morocco, yupo kwenye mbio za kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo ngumu zaidi Afrika, ambapo hadi sasa anashika nafasi ya pili nyuma ya Raja Casablanca akiwa na alama 68,  akizidiwa 1 tu na Raja.

Akichuku  kombe hilo anakuwa amejiandikia CV nzuri sana huko   Morocco,  licha ya kwamba tayari timu hiyo  ina uwezo wa kucheza Ligi ya mabingwa Afrika, kwa msimu ujao.

Akiwa Yanga kocha huyo aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo, kila moja na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kumpisha Miguel Gamondi aliyetetea ubingwa wa Ligi na Shirikisho, huku Ngao akiipoteza kwa Simba.

SOMA NA HII  TIKETI ZATOLEWA BURE KWA MASHABIKI LEO...MECHI YA TAIFA STARS VS UGANDA