Home Habari za michezo KUTOKA KAMBI YA YANGA….NABI AWAONYESHA UTEMI MASTAA WAPYA YANGA….AWAKIMBIZA KAMA ‘WATOTO’ MCHANA...

KUTOKA KAMBI YA YANGA….NABI AWAONYESHA UTEMI MASTAA WAPYA YANGA….AWAKIMBIZA KAMA ‘WATOTO’ MCHANA KWEUPEE..


Yanga kuna kazi ya kibabe inaendelea pale kambini kwao Avic, Kigamboni na huko hakuna kucheka ni dozi kali wachezaji wakijifua chini ya makocha wao, lakini sasa kuna mabadiliko ya dozi hiyo.

Katika kambi hiyo ya mazoezi ambayo ilianza juzi, timu hiyo imetumia siku mbili kufungua mapafu wakikimbia huku wakichezea mpira kidogo.

Ratiba hiyo ilianzia juzi jioni huku mastaa wapya watano Stephane Azizi Ki, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana na Lazarous Kambole wakiwamo na dozi ya mbio iliendelea na juzi asubuhi.

Hata hivyo, kocha mkuu Nasreddine Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze ambao wanafanya kazi hiyo na kocha wa mazoezi ya viungo Helmy Gueldich jana walibadilisha ratiba wakiongeza dozi zaidi.

SOMA NA HII  FEI TOTO LEO NDIO LEO ASEMA HAYA KUITIFUA YANGA