Home Habari za Yanga Leo AZIZ KI AMUAMSHA AMIS TAMBWE…MVP WA LIGI KUU?

AZIZ KI AMUAMSHA AMIS TAMBWE…MVP WA LIGI KUU?

AZIZ KI

REKODI ya mabao 21 aliyofunga Stephen Aziz Ki msimu 2023/24 imeonekana kumshtua mshambuliaji wa zamani wa Yanga Amis Tambwe, na kutuma ujumbe wake kwa mchezaji huyo Raia wa Burkina Faso.

Aziz Ki amefanikiwa kuifikia rekodi ya Amis Tambwe aliyoiweka msimu 2015/2016 alipofunga mabao 21 na rekodi hiyo imedumu kwa misimu minane ndani ya kikosi hicho.

Baada ya kiwango kizuri kuoneshwa na mchezaji huyo, ambaye pia anapewa nafsi kubwa ya kuchukua tuzo ya MVP wa Ligi kuu ya NBC, Tambwe alisema;

“Kwangu nampongeza sana (Aziz Ki) kwa sababu sio rahisi tena kwa mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo uwanjani. Anastahili heshima kubwa kwa sababu wapo washambuliaji wengi wakubwa na wakali walipita Yanga ila walishindwa hata kuisogelea,” alisema.

Amis Tambwe msimu 2013-2014 akiwa katika kabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC, aliibuka mfungaji bora akifunga jumla ya mabao 19.

Katika kunogesha mazungumzo yake Tambwe hakusita kuweka wazi kwmba, Aziz Ki kwake ndiye mchezaji bora wa msimu kutokana na mchango mkubwa aliouonyesha.

“Sina shaka kama atachaguliwa mchezaji bora wa msimu (MVP), kwa sababu mabao mengi aliyofunga yameisaidia Yanga kufikia malengo iliyojiwekea, nawapongeza wote walioonyesha kiwango kizuri msimu huu ila Aziz Ki kwangu ndiye amenikosha zaidi.”

Mbali na Tambwe kuzichezea Yanga, Simba ila timu nyingine aliyoichezea hapa nchini ni Singida Fountain Gate aliyoondoka mwaka 2022.

SOMA NA HII  SAKATA LA FEI TOTO...YANGA WAAMUA KAMA 'MBWAI NA IWE MBWAI'...WAMPIGA BEI....