Home Habari za Yanga Leo YANGA YAPIGA HESABU KALI FA…MASHABIKI HUMU TU

YANGA YAPIGA HESABU KALI FA…MASHABIKI HUMU TU

Habari za Yanga Leo

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Yanga SC wameanza kupiga hesabu kali kuelekea mchezo wao wa fainali dhidi ya Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tayari kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kilitia visiwa vya karafuu Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wa fainali unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Juni 1, katika uwanja New Amaan.

Ukiweka kando kuwa na taji la ligi Yanga wanapiga hesabu za kutwaa taji hilo ambalo wanalitetea kwa kuwa walitwaa mbele ya Azam FC fainali ya Tanga, Uwanja wa Mkwani.

ITAKUWA NI FAINALI YENYE TUZO ZA LIGI KUU YA NBC

Kwenye fainali inatarajiwa pia tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa wachezaji walioshiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 kutolewa pia baada ya fainali.

Miongoni mwa tuzo ambazo zinapigiwa hesabu kubwa ni ile ya MVP ambapo majina ya wachezaji wawili Feisal Salum wa Azam na Aziz KI wa Yanga yanatajwa kuwa miongoni mwa wale ambao wataibuka na tuzo hiyo kubwa.

Bakari Mwamnyeto, nahodha wa Yanga amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo huo kwa kuwa tayari maandalizi yameanza.

“Tupo tayari kwa fainali na si asilimia 100 ni asilimia elfu moja, maandalizi yapo sawa na tunaamini kwamba tunakwenda kulitetea taji.”.
Fainali inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Juni 2 2024.

SOMA NA HII  HUKU USAJILI UKIFUNGWA..... GAMONDI ASHUSHA NONDO 5 YANGA, AMUONDOA SKUDU......AWAONYA WALIOITWA TAIFA STARS