Home Ligi Kuu KMC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

KMC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA


 CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga. 

Mchezo huo ambao ni wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.

Walipokutana Uwanja wa CCM Kirumba mzunguko wa kwanza ubao ulisoma, KMC 1-2 Yanga hivyo utakuwa ni mchezo wa kulinda rekodi kwa Yanga na kisasi kwa KMC.

Christina amesema:”Kila kitu kipo sawa na wachezaji wanahitaji kufanya vizuri ili kupata pointi tatu,mazoezi ambayo wanayafanya yanaamanisha kwamba wanahitaji ushindi.

“Benchi la ufundi linafanya kazi kwa usawa ili kuona namna gani vijana wanaweza kuibuka na ushindi kwenye mechi yetu dhidi ya Yanga pamoja na mechi nyingine,” ,

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 50, KMC ipo nafasi ya tano na pointi zake ni 35.


SOMA NA HII  MASAU BWIRE:NIOMBEENI,NIMEAMBIWA NIMEKULA CHAKULA CHENYE SUMU