Home Habari za michezo YANGA WATIKISA MBUYU NIGERIA….WAKIVUKA TU KUKUTANA NA VIGOGO HAWA NUSU FAINAL CAF…

YANGA WATIKISA MBUYU NIGERIA….WAKIVUKA TU KUKUTANA NA VIGOGO HAWA NUSU FAINAL CAF…

River vs Yanga SC

TIMU ya Yanga SC imeanza vyema hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Godswill Akpabio.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria, shujaa wa Yanga SC aliyeipa furaha ni mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Fiston Mayele aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 73 na 81.

Katika michezo 15 ya CAF ambayo Rivers imecheza ikiwa nyumbani huu unakuwa ni mchezo wa pili kwao kupoteza baada ya awali kufungwa bao 1-0 na Far Rabat ya Morocco ikishinda 12 na sare dhidi ya Disables Noirs.

Miongoni mwa timu ambazo Rivers imewahi kuzifunga ikiwa nyumbani ni Enyimba, Club Africain, Asec Mimosas, El Merrick, Wydad Casablanca na Bloemfontein.

Katika michezo 11 iliyopita ya mashindano ya Klabu Afrika ambayo Rivers United imecheza nyumbani imeshinda minane, sare miwili na kupoteza mmoja ikifunga jumla ya mabao 33 na kuruhusu manane.

Kwa upande wa Yanga SC katika michezo 11 ikicheza ugenini imeshinda mitano, sare mmoja na kupoteza mitano ikifunga mabao 11 na kuruhusu 10.

Yanga imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwani katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 30 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam inahitaji sare tu.

Endapo Yanga itafuzu hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya Pyramids (Misri) au Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambapo mechi yao jana iliisha kwa sare ya 1-1 nchini Misri.

SOMA NA HII  SIMBA SASA TUACHE KUJIFARIJI..... NJIA NI HII TU