Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SINGIDA KESHO….SIMBA KUINGIA CHAMAZI KIMACHALE MACHALE…ISHU IKO HIVI…

KUELEKEA MECHI NA SINGIDA KESHO….SIMBA KUINGIA CHAMAZI KIMACHALE MACHALE…ISHU IKO HIVI…

Habari za Simba leo

KIKOSI cha Simba kesho kinatarajiwa kushuka kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, saa 12:00 jioni kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Singida Fountain Gate FC,

Katika mchezo huo Simba watakuwa nyumbani Azam Complex baada ya uwanja wa Jamhuri Morogoro kufungiwa kutokana na kutokidhi na vigezo vya Bodi la Ligi nchini.

Timu hizo zote zinakutana kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara bila kuwa na makocha wake wakuu benchini, Abdelhak Benchikha akienda kuongeza ujuzi kwa kufanya kozi fupi na kuwaachia wasaidizi wake kikosi kikiongozwa na Selemani Matola, huku Singida Fountain Gate FC ikiwa imetimua benchi lote la ufundi na kupewa ukaimu Ngawina Ngawina kuingoza kikosi cha timu hiyo.

Kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amesema maandalizi ya mechi ya kesho yamekamilika na  Singida Fountain Gate FC, siku zote hakuna mechi rahisi lakini wamejipanga kwa ubora na madhaifu ya wapinzani wao.

Amesema itakuwa mechi ya ushindani, Singida Fountain Gate FC inawatapa wakati mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna pointi tatu katika mchezo wa leo.

“Tumechukuwa tahadhari kubwa katika safu yetu ya ulinzi kwa sababu tukifanya makosa katika nafasi hiyo kwa timu ya Singida Fountain Gate FC basi tunaweza kupoteza

Kulingana na ratiba tuliyokuwa nayo tutakuwa na mabadiliko ya kikosi kwa kuwapa nafasi ya wachezaji wengine kupumzika na wale wahakucheza mechi mbili zilizipita watapata nafasi,” amesema Matola.

Kaimu Kocha wa Singida Fountain Gate, Ngawina Ngawina amesema wamefanya maandalizi ya mwisho wanaifahamu Simba wamejipanga kulingana na ubora wa wapinzani wao kuhakikisha wanaonyesha mchezo mzuri.

Amesema anakiri katika michezo minne hawajapata matokeo mazuri lakini anaendelea walipoishia wenzake waliopita kuhakikisha wanamaliza dakika 90 kwa kutafuta alama muhimu.

“Tutacheza kwa tahadhari kubwa sana kwa sababu tunafahamu ubora wa Simba ikiwemo safu yake ya ushambuliaji lakini pia kuna madhaifu yao katika ulinzi tukiwa makini tutawafurahisha mashabiki wetu,” amesema Ngawina.

Nahodha wa Singida Fountain Gate FC, Beno Kakolanya amesema wanaifahamu Simba na wataenda kucheza mechi hiyo kwa tahadhari kubwa kwa kutafuta pointi ili kujiweka katika nafasi nzuri.

“Niliwahi kucheza Simba hiyo sio kigezo kwetu kikubwa nawafahamu wapinzani wetu na kuingia kwa tahadhari kubwa ili kuweza kuvuna pointi tukikosa tatu basi tupate moja,” amesema Kakolanya.

SOMA NA HII  KISA MATOKEO YA SARE JANA...AHMED ALLY AIITA YANGA 'WACHAWI UNITED'...ADAI WAMEFUKIA HIRIZI...