Home Habari za Simba Leo MO DEWJI AKUBALI KURUDI SIMBA…AANZA NA JINA HILI KUSAJILI

MO DEWJI AKUBALI KURUDI SIMBA…AANZA NA JINA HILI KUSAJILI

Habari za Simba

INAELEZWA kwamba Rais wa heshima na muwekezaji   wa klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji  (MO Dewji) amekubali kufanya kazi kwa karibu zaidi na Uongozi wa klabu hiyo, ukiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah Lihenye “Try Again”.

Awali kulikuwa na taarifa zikisema kwamba, MO Dewji amesusa kutoa pesa za uendeshaji wa klabu hiyo, hali hiyo imepelekea Simba kutofanya vizuri katika mashindano ya ndani na ya Kimataifa, Ligi ya Mbingwa Afrika kwani waliweka malengo ya kufika hatua ya Nusu Fainali.

Moja ya chanzo cha habari cha kuaminika kutoka kwa mtu wa karibu zaidi na Uongozi wa Simba alinukuliwa akisema kwamba;

“MO Dewji alijitoa na kujiweka mbali zaidi na Simba kwa muda mrefu sasa, amekuwa hatoi pesa za uendeshaji wa klabu”

“Kwa mwezi imba inalipa mishahara wachezaji na wafanyakazi wengine takribani Tsh Milioni 600/=, yote hiyo inatoka kwenye vyanzo vingne vya mapato, Azam Media wanatoa Tsh 200,mdhamini mkuu wa timu anatoa Tsh M200/=, Wadhamini wengine wanatoa Tsh Mil 100/= jumla inakuwa Tsh Mil 500/= inabaki deni la Mil 100/=”

Chanzo hicho cha habari kiliendelea  kusema kwamba, ” Simba imekuwa ikiendeshwa kwa pesa za “Treasury Bond” na MO Dewji wala hajaweka ile Bil 20/= TZS kwenye akaunti ya Simba, bali ipo kwenye akaunti yake, kwahiyo faida inayopatikana kwa mwaka kama Tsh Bil 3 ndiyo hiyo amekuwa akiitoa kwaajili ya Simba SC.”

Takribani misimu   mitatau sasa Simba SC imekuwa ikipitia hali ngumu kiutendaji, huku sababu kubwa ikionekana ni mpasuko mkubwa na makundi yaliyopo ndani ya Uongozi wa klabu hiyo.

Katika Dirisha hili la usajili Simba imeanza na mchezaji wa AS Vita Club Elie Mpanzu, winga hatari  aliyefunga jumla ya magoli 11 msimu kwenye ligi kuu ya nchini DR Congo.

SOMA NA HII  YANGA KILA KITU NI FRESH, BADO WENYE NCHI