Home Habari za michezo YANGA KILA KITU NI FRESH, BADO WENYE NCHI

YANGA KILA KITU NI FRESH, BADO WENYE NCHI

Habari za Yanga

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki mbio za NBC Marathoni huku akisema kilele cha wiki ya Wananchi kimepita inayosubiriwa ni siku ya wenye Nchi.

Jumamosi ,Julai 22,2023 klabu ya Yanga ilihitimisha kilele cha wiki ya mwananchi kwa kucheza na Kaizer Chief ya Afrika Kusini katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Kennedy Musonda.

Akizungumza leo Jumapili Julai 23 katika mbio za NBC Marathoni katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa Majaliwa amesema baada ya mchezo wa jana sasa kinachosubiriwa ni siku ya Simba Day Agosti 6 mwaka huu.

“Niwakumbushe jana ilikuwa siku ya wananchi, Yanga inajiandaa kuingia katika ligi kuu,sasa tarehe 6 ni siku ya wenye nchi,nao wanajindaa, kuna wenye nchi na wananchi lakini kuna Azam, Namungo na Singida Big Stars hii yote ni hamasa iliyotolewa na NBC,”amesema Majaliwa

Waziri Mkuu ameipongeza benki ya NBC kwa kuandaa mbio huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano huo.
Amesema Serikali inahitaji kuona kila taasisi ikipambana kuhakikisha sekta ya afya inazidi kuboreka nchini.

“Nitumie nafasi hii kuipongeza NBC kwa kuendeleza michezo piga makofi kwa NBC, watanzania mnajua benki hii ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu ambayo ni ligi maarufu na inachukua nafasi ya tano, hizi ni jitihada za NBC,”amesema Waziri Mkuu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kupitia mbio hizo jumla ya Sh300 milioni zimepatikana na zitaenda moja kwa moja kwenye matibabu ya kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kwenye taaluma ya ukunga nchini.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoPindi Chanaamesema wamedhamiria kuwaondoa wagonjwa kwenye vitanda kwa kutumia mfumo wa ufanyaji mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa.

SOMA NA HII  YANGA IMERUDI KWA KAZE, YAMPA OFA HIZI HAPA MBILI SIO POA