Home Uncategorized MEDDIE KAGERE ATAJA SABABU INAYOMPONZA ASHINDWE KUFUNGA KWENYE BAADHI YA MECHI BONGO

MEDDIE KAGERE ATAJA SABABU INAYOMPONZA ASHINDWE KUFUNGA KWENYE BAADHI YA MECHI BONGO


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba ambaye ni kinara wa kutupia ndani ya ligi amesema kuwa sababu kubwa iliyokuwa ikimfanya ashindwe kufunga kwenye mechi za hivi karibuni ni kubanwa na mabeki muda wote.

Kagere ametupia mabao 14 kati ya 50 yaliyofungwa na Simba, hakufurukuta kwenye baadhi ya mechi ambazo Simba ilicheza mfululizo.

Mechi hizo ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Uhuru Simba ilichapwa bao 1-0, Mtibwa 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba, alikuja kuibukia mbele ya Kagera Sugar alifunga kwa penalti na mchezo wao dhidi ya Biashara United alifunga pia.

Kagere amesema:-“Nimekuwa nikipambana kwa ajili ya timu na wachezaji wenzangu, wote tunashirikiana na kufanya kazi tukiwa ni timu, kinachonifanya kwenye baadhi ya mechi kutofunga ni mabeki wengi kunitazama na kunifuatilia muda wote”.

SOMA NA HII  KAZE KUANZA NA HESABU HIZI KWA POLISI TANZANIA