Home news ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI YANGA WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA

ORODHA YA MAJINA YA WACHEZAJI YANGA WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA


IKIWA inajiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya River United ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Septemba 12, tayari mabosi hao wametuma orodha ya wachezaji watakaowatumia kimataifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 11:00 jioni, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni wa hatua ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hiki hapa kikosi cha Yanga ambacho kitakuwa na kazi ya kufanya katika mashindano ya kimataifa:-

 Eric Johora,Ramadhan Kabwili na Djigui Diarra kwa upande wa walinda mlango.

Mabeki wa pembeni ni Shaban Djuma,Kibwana Shomari,Paul Godfery,Yassin Mustapha,Adeyum Saleh, David Bryson,Litombo, Dickson Job,Bakari Mwamnyeto na Abdallah Shaibu,’Ninja’.

Viungo ni Mukoko Tonombe, Feisal Salum,Khalid Aucho,Zawad Mauya,Farid Mussa, Deus Kaseke,Mapinduzi Balama na Dickson Ambundo.

Washambuliaji ni Heritier Makambo,Mayele,Ditram Nchimbi na Yusuph Athuman.

SOMA NA HII  TAKWIMU ZINAONGEA....LOMALISA AANZA KUILIPA YANGA SC...KAZI YAKE SI YA KITOTO...