Home Makala SURA YA KAZI, KIUMBE ANAYETAJWA KUTWAA MATAJI MENGI

SURA YA KAZI, KIUMBE ANAYETAJWA KUTWAA MATAJI MENGI


SURA ya kazi, sura ya tabasamu lake ushindi, sura ya ukubwa ndani ya uwanja kwa zama zake si mwingine ni kiungo fundi anayejua kucheza na kuwapa furaha mashabiki zama zile akiwa ndani ya uwanja anaitwa Ryan Joseph Giggs.


Novemba 29,1973 aliletwa duniani na maisha yake ya soka amecheza muda mrefu ndani ya Manchester United ya Uingereza na alipata muda wa kuwa Kocha Mkuu kwa muda baada ya David Moyes kufutwa kazi mazima ilikuwa ni Aprili 2014.

Alistaafu rasmi soka la ushindani Mei 19,2014 na nyota huyo ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Wales alicheza jumla ya mechi 64 kwenye timu hiyo kuanzia 1991 mpaka 2007.

Ndani ya Ligi Kuu England amecheza jumla ya mechi 632 na alitupia mabao 109 pasi 161, katika Ligi ya Mabingwa Ulaya alicheza jumla ya mechi 145 na alifunga mabao 28 na alitoa pasi 46.

Rekodi zinaonyesha kuwa katika ngazi ya klabu ni jumla ya mechi 932 alicheza na mabao ni 163 ambayo alitupia na pasi 250 za mabao kwa kiungo huyo aliyecheza mechi nyingi ndani ya Manchester United.

Ana mataji 13 ya Ligi Kuu England, mataji manne ya FA, Football League Cup mataji matatu, Ngao ya Jamii mataji 9 na UEFA Super Cup taji moja ilikuwa ni mwaka 1991, taji moja la FIFA Club World Cup ilikuwa ni 2008.

Ni kiumbe ambaye anatajwa kuweza kunyanyua mataji mengi na maisha yake ya mpira ametumia muda mwingi ndani ya Manchester United.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUA RUVU SHOOTING...ALLY SONSO ASIMULIA ALIVYOFUKUZWA YANGA..AMTAJA ZAHERA