Home kimataifa POGBA ATUPIA MABAO 28 NDANI YA MANCHESTER UNITED

POGBA ATUPIA MABAO 28 NDANI YA MANCHESTER UNITED


KIUNGO Paul Pogba raia wa Ufaransa amecheza jumla ya mechi 137 ndani ya Ligi Kuu England ambapo kwa sasa ni mali ya Manchester United.

Katika mechi hizo ambazo amecheza rekodi zinaonyesha kwamba amefunga jumla ya mabao 28 na kutoa pasi 29.

Winga huyo ameletwa duniani Machi 15 1993 ana umri wa miaka 28 ambapo kwa sasa amegoma kuongeza dili jipya ndani ya Manchester United.

Nyota huyo aliibuka ndani ya kikosi hicho msimu wa 2016 akitokea Klabu ya Juventus ambayo inashiriki Serie A.

Akiwa huko ndani ya Juventus, rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 124 na alitupia mabao 28.

Hivyo raia huyo wa Ufaransa ambaye ameshinda taji a Kombe la Dunia ni mzee wa kutupia mabao 28 katika maisha yake ndani ya timu ambazo amecheza mpaka sasa.

SOMA NA HII  LUKAKU KUIBUKIA CHELSEA