Home kimataifa LUKAKU KUIBUKIA CHELSEA

LUKAKU KUIBUKIA CHELSEA


MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku ambaye alisepa ndani ya Klabu ya  Chelsea mwaka 2014 na kwa sasa anakipiga ndani ya Inter Milan amewaambia mabosi wake kwamba wamruhusu aondoke ikiwa atapata ofa nzuri mezani.

Nyota huyo amefunga jumla ya mabao 24 na timu hiyo ya Inter Milan  ilitwaa taji la  Serie A msimu uliopita na inaelezwa kuwa Chelsea wapo mezani kufanya mazungumzo ili kumpata mchezaj wao wa zamani.

Dau ambalo wameweka mezani kwa ajili ya kupata saini yake ni pauni milioni 97.5 jambo ambalo linaonesha kwamba anaweza kuondoka hapo huku habari zikieleza kuwa tayari kila kitu kinakwenda sawa.

Kutokana na dau kuwa nono imekuwa ngumu kwa Inter Milan kugomea ishu hiyo jambo ambalo limepelekea aandaliwe mkataba wa miaka mitano baada ya kufanyiwa vipimo kwa raia huyo wa Ubelgiji ambapo awali Inter Milan walikataa ofa ya pauni milioni 80.


SOMA NA HII  BENZEMA AFIKISHA MABAO 71 UEFA, ZIDANE MATUMAINI KIBAO