Home Simba SC SIMBA WABADILI GIA ANGANI..SASA KUONYESHANA UBABE NA YANGA MOROCCO

SIMBA WABADILI GIA ANGANI..SASA KUONYESHANA UBABE NA YANGA MOROCCO


MABINGWA wa Ligi Kuu Bara Simba huenda wakabadili mawazo ya eneo watakaloweka kambi yao ya maandalizi ya msimu, wakifikiria kwenda Ufaransa, ila kutegemea na uamuzi wa Kocha Mkuu wao, Didier Gomes kama atachomoa pendekezo lao la kuweka kambi yao nchini Morocco badala ya Misri.

Awali Simba ilipanga kwenda Misri katika Mji wa Alexandria kutokana na pendekezo la Gomes na fasta mabosi wa klabu hiyo walianza mchakato wa kulikamilisha hilo ikiwemo kuomba visa.

Inaelezwa mabosi hao wa Simba, wamebadili mawazo na wanaweza kuweka kambi Morocco kwani taratibu za kuingia humu si ngumu na kila kitu kinapatikana kwa haraka ikiwemo hoteli, eneo ambalo watafanyia mazoezi mbalimbali na mambo mengine ya msingi. Mabosi hao wa Simba ambalo wamelipanga wakati huu ni kumueleza (Gomes), kuwa upatikanaji wa mahitaji ya msingi, Morocco ni rahisi kuliko kule Misri alipo pendekeza awali.

“Tutamueleza kutokana na mazingira yalivyo Morocco tumeona ni bora zaidi kutokana vitu vyote vya msingi ambavyo alikuwa anahitaji vinapatikana kwa uarahisi,” alisema mtoa taarifa na kuongeza;

“Kama atakubaliana na jambo hili la kwenda Morocco itakuwa vizuri itakuwa rahisi hata kwake kutoka Ufaransa kuingia nchini humu kwani ni karibu lakini kama atapendelea Misri zaidi inabidi tupambane ili kulitimiza hilo.”

Katika kipindi cha miaka minne katika kikosi cha Simba tangu kuingia kwa Mwenyekiti wa bodi, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ wamekuwa wakibadilisha nchi mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya msimu.

Mo Dewji ameipeleka Simba, Uturuki, Afrika Kusini mara mbili na awali hii kama si Morocco basi watakwenda Misri na hapo ambacho kinasubiriwa ni maamuzi ya Gomes tu.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema maandalizi ya msimu yatafanyika kama ilivyo kawaida yao na hilo linategemea benchi lao la ufundi litakuwa linahitaji eneo gani sahihi.

SOMA NA HII  WANACHAMA SIMBA WAITWA KUCHUKUA FOMU ZA UBOSI WA BODI YA WAKURUGENZI...