Home Uncategorized Shomari Kapombe bado yuko Simba

Shomari Kapombe bado yuko Simba

Usajili wa klabu ya Simba unaendelea, ambapo leo kupitia mitandao yao ya kijamii wamedhibitisha kumpa mkataba mpya beki wao wa kulia Shomari Kapombe.

Shomari Kapombe amepewa mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo. Shomari Kapombe bado anafanya mazoezi ya kurudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kutoka kwenye majeraha.

Beki huyo alipata majeraha akiwa na timu ya taifa , taifa stars katika kambi ya timu hiyo iliyokuwa nchini Afrika kusini kujiandaa na mechi ya kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho.

The post Shomari Kapombe bado yuko Simba appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA ONYO MAPEMA KABISA BAADA YA KUSHINDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here