Home Uncategorized HUU HAPA USHAURI WA SALEH JEMBE KWENDA SIMBA, YANGA YATAJWA

HUU HAPA USHAURI WA SALEH JEMBE KWENDA SIMBA, YANGA YATAJWA


KUTOKANA na kichapo cha bao 1-0 walichopokea Simba mbele ya JKT Tanzania jana, Februari 7,2020 kupokelewa kwa mtindo wa kipekee kwa mashabiki na viongozi.

Huu hapa ushauri wa Saleh Jembe kwa Simba:-Nimesikia kiongozi mmoja wa Simba akilia kuwa ndani yao kuna hujuma. USHAURI WANGU :- Wawe watulivu, Papara za namna hiyo kama anazoonyesha kiongozi huyo zimekuwa ADUI mkubwa wa Simba mara kadhaa.

Kwani Simba ni nani asifungwe. Kama kuna jambo walishughulikie huko na si kulalama hadharani. Akishindwa anaweza kusema watu wamuelewe.

Yanga walionyesha weledi, walifungwa mechi 2 mfululizo, WAKATULIA, wakajipanga na KURUDI mchezoni.Leo wanafanya vema. Huenda hao viongozi wa Simba wanaweza KUJIFUNZA hapo na kupunguza UJUAJI uliopindukia.

SOMA NA HII  VIDEO: KOCHA WA SIMBA AZUNGUMZIA KUHUSU MIPANGO YAKE, KESHO KUANZA MAZOEZI