Home Uncategorized KUMEKUCHA MWADUI FC, KUSUKA KIKOSI KIPYA CHA KUTISHA

KUMEKUCHA MWADUI FC, KUSUKA KIKOSI KIPYA CHA KUTISHA


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kusuka kikosi kipya kitakacholeta ushindani mkali msimu ujao baada ya kubaki kwenye Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na Salehe Jembe, Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao amesema kuwa baada ya kubaki kwenye ligi mpango wa kwanza ni kusuka kikosi upya.

“Tumenusurika kushuka daraja kutokana na kushindwa kumudu ushindani kwa msimu uliopita, kwa sasa tunaangalia namna bora itakayotufanya tuwe bora kwenye ushindani msimu ujao.

“Kikosi makini na chenye nguvu tutakuwa nacho msimu mpya hivyo mashabiki na wadau waendelee kutupa sapoti kama ambavyo walikuwa nasi bega kwa bega kwenye mchezo wetu wa playoff dhidi ya Geita,” amesema.
SOMA NA HII  FIFA KUMPA TUZO YA HESHIMA NYOTA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON