Home Habari za michezo KISA KOSA KOSA ZA KINA KAGERE,….KOCHA SIMBA KAAMUA KUWATOLEA UVIVU…AFUNGUKA WALICHOFANYIWA…

KISA KOSA KOSA ZA KINA KAGERE,….KOCHA SIMBA KAAMUA KUWATOLEA UVIVU…AFUNGUKA WALICHOFANYIWA…


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba, amesema wanayafanyia kazi makosa ya wachezaji wao ikiwa ni pamoja na tatizo la umaliziaji wa nafasi wanazozipata.

Wakati Simba ikishinda 1-2 dhidi ya Coastal Union Alhamisi wiki hii, wachezaji wa timu hiyo walikosa nafasi 10 za kufunga akiwemo Chris Mugalu, Meddie Kagere, Bernard Morrison na Clatous Chama.

Mabingwa hao watetezi kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara wapo nafasi ya pili wakiwa wameachwa pointi 11 na Yanga iliyo nafasi ya kwanza. Leo Jumapili watacheza dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, Kilimanjaro.

Matola alisema: “Makosa yapo kwenye mechi ambazo tunacheza, tunaona kwamba hata mchezo wetu dhidi ya Coastal Union tulipoteza nafasi nyingi, hivyo tunalifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi, muda si mrefu mambo yatakuwa sawa,” alisema.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA KARIAKOO...MBRAZILI SIMBA 'AMPUMBAZA' GAMONDI MBELE YA WANAHABARI...