Home Azam FC AGREY MORRIS AFUNGUKA PATASHIKA YAKE NA MAYELE…ADAI MPIRA SIO UHASAMA….

AGREY MORRIS AFUNGUKA PATASHIKA YAKE NA MAYELE…ADAI MPIRA SIO UHASAMA….

Beki tegemeo wa Azam FC, Aggrey Morris amekiri kwa mdomo wake kuwa, Fiston Mayele wa Yanga analijua lango. Mayele alifunga bao la ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam juzi usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Aggrey na mwenzie Abdallah Kheri ‘Sebo’ walikuwa na bato la hatari dhidi ya Mayele kuhakikisha hafungi au kuleta madhara langoni mwa Azam na kazi hiyo waliifanikisha kwa dakika 77 tu. Baada ya hapo straika huyo akawazidi akili na kutetema baada ya kutupia dakika ya 78 akiunganisha krosi ya Djuma Shaban na kumuacha kipa Ahmed Salula akiokota mpira nyavuni.

Staa huyo alikiri Mayele anafanya kazi yake kama straika na hakuona shida kumpongeza kwa bidii aliyoionyesha kuitetea timu yake, ipate pointi tatu.

“Soka ndivyo lilivyo, Mayele kapambana kafunga, upande wangu nilipambana kuilinda timu yangu ila Yanga wakatumia mapungufu yetu kutuadhibu, hatuwezi kuishia hapo tunajipanga kwa mechi zijazo,” alisema Aggrey na kuongeza;

“Mayele anajua kufunga na hakati tamaa, yote katika yote mpira sio uhasama nimpongeze kisha maisha mengine yaendelee.”

Mfungaji wa bao la Azam, Rodgers Kola aliyemtungua kipa wa Yanga, Djigui Diarra dakika ya 10 akipokea asisti ya Bruce Kangwa, alisema japo wamezikosa pointi tatu, ila waliupiga mpira mwingi.

Kola aliyefikisha bao la tano, alisema matokeo ya soka hayaangalii nani kacheza vizuri, ila nani anamaliza kwa ushindi ili kuzipata pointi tatu muhimu.

“Sijaona kama Yanga imecheza sana kuliko sisi, tumejituma sana, ila kwenye mpira kosa moja linakuadhibu ndicho ilichokifanya Yanga,” alisema.

Bao la juzi limemfanya Mayele kuwa kinara akifikisha mabao 11 akimuacha Reliants Lusajo wa Namungio wenye 10.

SOMA NA HII  YANGA WAAMUA AISEEE...WAPELEKA 'FULL KIKOSI' ALGERIA...MASTAA WOTE MPAKA MAJERUHI WAENDA...