Kikosi cha Yanga kimeondoka katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere kuelekea Algeria kwa ajili ya mechi ya mkondo wa pili dhidi ya USM ALGER Jumamosi Juni 3, 2023.
Mechi ya kwanza ya fainalo ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 2-1 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga imeondoka na Ndege ya Serikali waliyopewa na Rais Samia Saluhu ikiwa na kikosi cha wachezaji 29, benchi la ufundi na viongozi mbalimbali waandamizi wa klabu hiyo pamoja na mashabiki.
Yanga watakuwa ni kibarua kigumu cha kubadilisha upepo wa matokeo , huku wakiamini kuwa historia yao ya kufanya vizuri kwa mechi za ugenini kwa msimu huu inaweza kuwabeba.
Ili kubadilisha matokeo Yanga, wanahitaji ushindi wa kuanzia magoli 2 na kuendelea mbele, huku pia wakiomba wapinzani wao wasipate goli lolote.
Kikosi cha Nabi, kinatazamia kuweka historia ya kipekee katika soka la ukanda wa Afrika Mashariki, endapo watafanikiwa kubeba ubingwa wa michuano hiyo namba tatu kwa thamani Afrika nyuma ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aidha, ushindi si tu utawapa Yanga pesa ya maana, pia utawapa nafasi ya kushindania taji lingine kubwa zaidi la CAF Mwanzoni mwa msimu ujao ikiwa ni taji la kufungua mashindano ya msimu ujao.