Home Geita Gold FC ILE ISHU YA USAJILI WA MJAPAN KWA GEITA GOLD ..MAMBO YOTE YAKO...

ILE ISHU YA USAJILI WA MJAPAN KWA GEITA GOLD ..MAMBO YOTE YAKO HIVI KUMBE…MINZIRO AFUNGUKA A-Z UKWELI WA MAMBO…


Kocha Mkuu wa Geita Gold, Fred Felix Minziro, amesema wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vya nyota wao, Shinobu Sakai raia wa Japan, tayari kwa kuanza kumtumia kwenye mechi za Ligi Kuu na mashindano mengine.

Geita Gold ambayo inajiandaa na mashindano ya kimataifa ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu zilizosajili nyota wa kimataifa kwa lengo la kuleta ushindani.

Akizungumza, Minziro alisema, anaimani kubwa na Mjapan wake pindi atakapoanza kuitumikia timu hiyo, na kudai kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vyake vya kufanya kazi nchini ili kuanza kutumika.

“Tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha vibali vya mchezaji wetu Shinob, hakuweza kucheza mechi za awali kwa kuwa hakuwa na kibali cha kazi na makazi, hivyo tunakamilisha utaratibu ili aweze kucheza.

“Ninamatumaini makubwa akianza kucheza kikosi kitakuwa kizuri pale atakapozoeana na wachezaji wenzake, lengo letu tunahitaji kuwa na kikosi bora cha ushindani msimu huu kuliko ulivyokuwa msimu uliopita,” alisema Minziro.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGA JUZI....PHIRI ATANGAZA HATARI KWA MABEKI LIGI KUU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here