Home Uncategorized MARTIN APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA BARCA

MARTIN APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA BARCA


STRAIKA wa Barcelona, Martin Braithwaite  amesema anataka kukaa ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ya mkataba ambao anao kwa sasa kwa kuhakikisha ainafanya klabu  hiyo kuwa bora zaidi.
Braithwaite amejiunga na Barcelona akitokea Leganes katika usajili wa dharura msimu huu hii ni baada ya Barca  mastaa wake Luis Suarez na Ousmane Dembele kutupwa nje kutokana na majeruhi.
 Straika  huyo ameingia mkataba na Barcelona ambao utadumu mpaka mwaka 2024 kuitumikia klabu hiyo.
 Straika   huyo amesema: “Ninahakika kuwa nitakaa hapa Barcelona kwa muda mrefu zaidi ya hata mkataba wangu.
“Nataka kuwa kucheza na kutwaa makombe sababu ni malengo yetu na kuja hapa ni wakati wangu muafaka mimi kuweka biidi na kuwa msaada.
 “ Hapa naangalia  wale malegendari walifanya nini katika klabu  kuangalia yale  mazuri ambao walifanya na kuacha alama  katika klabu ndiyo kitu kizuri ambacho hata mimi  hapa tajifunza kupitia kwa kwa kuhakikisha  na weka  alama hapa Barca hata vizazi vijavyo vijekuona kitu  ambacho nilifanya  nini hapa,”alisema.
 Straika huyo tangu ajiunge na klabu hiyo amecheza mechi  tatu za La Liga kabla ya kusimama kutokana na virusi vya corona amecheza dhidi ya Eibar, Real Madrid na Real Sociedad.
SOMA NA HII  ISHU YA MATOLA KUIBUKIA AZAM FC IPO HIVI