Home Habari za michezo KISA MSHAHARA KIDUCHU…..MANULA AIPIGA CHINI OFA YA AZAM FC…

KISA MSHAHARA KIDUCHU…..MANULA AIPIGA CHINI OFA YA AZAM FC…

Habari za Simba leo

Kipa namba moja wa Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania, Aishi Salum Manula amesema sababu ya kuondoka kwake Azam FC kwenda Simba ilikuwa ni baada ya mabadiliko ndani ya Wauza Ukwaju wa Dar ikiwa ni pamoja na kumpunguzia mshahara wake.

Manula amesema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Millard Ayo kuhusu maisha yake ya Soka.

“Mimi kuondoka Azam FC ilinibidi kwa sababu kilikuwa kipindi cha mabadiliko, aliletwa Meneja Mkuu ambaye alikuja na mifumo tofauti kabisa. Alikuja na sera ya kubana matumizi na mabosi wakamuamini kwa sababi matajiri wengi wanapenda ubanaji matumizi ili uendeshaji wa timu uwe wa gharama nafuu.

“Wakati anakuja alikuta watu wengine tunamaliza mikataba, kwa hiyo kama mtu unalipwa Tsh milioni 1.5 anataka ulipwe Tsh milioni 1, kama gharama yako ya usajili ilikuwa Tsh milioni 30 hapo nyuma, anataka gharama yako iwe Tsh milioni 15. Kutokana na ubora wetu tuliamini tunapaswa kulipwa zaidi ya hapo.

“Na ile haikuwa makubaliano, yalikuwa maamuzi ambayo meneja yule alikuja nayo, kwa hiyo hata wewe ukienda anakwambia huu mshahara ndio umewekewa kama unataka saini, kama hutaki acha. Hata kuongeza na bosi alinikatalia akataka niongee na yeye wakati mwanzo tulikuwa tunzungumza na bosi na mambo yanakuwa mazuri.

“Kwa hiyo ilipofikia hapo tukaamua kuondoka na kwenda Simba baada ya kupata dili lao, nilifurahi kwa sababu nakwenda kujiunga na timu yenye mashabiki wengi licha ya uwezo wa Simba kwa wakati ule walikuwa chini yetu sisi Azam, baada ya kubeba ubingwa 2024, tulikuwa tunamaliza nafasi ya 2 wakati Simba wakimaliza wanne,” amesema Manula.

SOMA NA HII  REKODI ZA,JEMBE JIPYA LA SIMBA KUTOKA NIGERIA