Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…YANGA HAITANIII AISEE…MCONGO MWINGINE ASHUSHWA USIKU USIKU…AZIZ KI NAYE NDANI…

KUELEKEA MSIMU UJAO…YANGA HAITANIII AISEE…MCONGO MWINGINE ASHUSHWA USIKU USIKU…AZIZ KI NAYE NDANI…


Hayawi hayawi sasa yamekua. Baada ya kuzungumzwa kwa muda mrefu hatimaye Mabingwa Tanzania 2021/2022 wamemtambulisha rasmi mlinzi wa kushoto raia wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Joyce Lomalisa Mutambala kujiunga na Wananchi kwa Mkataba wa miaka miwili.

Lomalisa anakuja Yanga katika wakati ambao mabingwa hao wa Tanzania wanasuka kikosi chao wakijiandaa kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Beki huyo wa kati anakuja Yanga kuungana na Wacongo wenzake katika kuipigania timu hiyo kwenye mashindano mbalimbali ya ndani na nnje ya  nchi.

Wachezaji wengine kutoka DR Congo ni pamoja na, Yannic Bangala, Fistoni Mayele, Jesus Moloko, Chico Ushindi. Herieth Makambo pamoja na Shabani Djuma.

Lomalisa anakuwa mchezaji wa nne mpya kutambulishwa ambapo tayari Yanga imewatambulisha, Kambole, Bigirimana pamoja na Stephen Aziz Ki.

SOMA NA HII  BIGIRIMANA AWASHA MOTO YANGA...ATAKA ALIPWE CHAKE ASEPE....MABOSI WAMUOMBA POO...