Home Habari za michezo RASMI….FIFA WAMTAJIRISHA MSUVA CHAP CHAP….WAARABU WAAMRIWA WAMLIPE BILIONI 1.6…ISHU NZIMA IKO HIVI….

RASMI….FIFA WAMTAJIRISHA MSUVA CHAP CHAP….WAARABU WAAMRIWA WAMLIPE BILIONI 1.6…ISHU NZIMA IKO HIVI….


Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza Club ya soka ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa Mchezaji Mtanzania Simon Msuva  zaidi ya dola za kimarekani laki saba (zaidi ya Tsh bilioni 1.6) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua  dhidi ya Club hiyo.

Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake December mwaka 202 kutokana na kuidai Club hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).

Aidha, imeelezwa kuwa hukumu ya FIFA imeamuru Mchezaji huyu alipwe na riba pia.

SOMA NA HII  MAYELE, BANGALA WAMVUTA JANGWANI NAHODHA WA TP MAZEMBE..MWENYEWE AANIKA KILA KITU...