Home Habari za michezo MKUDE AIBUA ‘ZONGO’ TIMU YA TAIFA….KOCHA TAIFA STARS AULIZWA MASWALI MAGUMU…

MKUDE AIBUA ‘ZONGO’ TIMU YA TAIFA….KOCHA TAIFA STARS AULIZWA MASWALI MAGUMU…

Taifa Stars

Kocha Mkuu wa Taifa Stars Adel Mrouche ametangaza kikosi cha Wachezaji 25 wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kitakachocheza dhidi ya Algeria katika mchezo wa kuwania kufuzu AFCON.

Kikosi hiko kimetangazwa huku majina ya Feisal Salum, Shomary Kapombe na Mohamed Hussein Zimbwe JR wakiachwa ila Clement Mzize na Jonas Mkude wamerejeshwa kikosini.

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Oscar Oscar hajakaa kimya, ametoa maoni yake kuhusu kuitwa kwa Mkude ambaye kwa sasa anakipiga Yanga.

“Nimeona orodha ya wachezaji ambao wameitwa timu ya Taifa na Kocha Mkuu Adel Amrouche kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kufuzu Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Algeria.

“Katika orodha hiyo hayupo kiungo shoka wa Singida Fountain Gate Yusuph Kagoma, ambaye amekuwa na uhakika katika kikosi hicho ambacho kwa sasa kina ushindani mkubwa wa wachezaji wa kigeni.

“Pia nimeona ameitwa kiungo wa Yanga Jonas Mkude ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza cha Yanga huku Yusuph Kagoma akiwa na uhakika wa kuanza moja kwa moja katika kikosi cha Singida Fountain Gate hajaitwa.

“Kocha ametumia kigezo gani kumuita Jonas Mkude na kumuacha Yusuph Kagoma ambaye msimu huu ana match fitness kubwa kuliko Mkude. Tangu michezo ya Ngao ya Jamii pale Tanga,Michuano ya Kimataifa na mechi za Ligi Kagoma amekuwa bora sana mbele Jonas Mkude.”

SOMA NA HII  KUHUSU TAARIFA ZA KUTAKA KUONDOKA ....ONYANGO AZIDI 'KUWAJAMBISHA' SIMBA....ADAI KAZI YAKE NI KUCHEZA MPIRA...