Home Habari za michezo KUHUSU KELELE ZA MASHABIKI KUWA YEYE NI ‘NYOKA LA KIBISA’….AZIZ KI AVUNJA...

KUHUSU KELELE ZA MASHABIKI KUWA YEYE NI ‘NYOKA LA KIBISA’….AZIZ KI AVUNJA UKIMYA…NABI AKAZIA ALIYOYASEMA …


Staa wa Yanga, Stephane Aziz Ki na Kocha wake, Nabi Mohammed wamesikia maneno ya wanaohoji kwanini mchezaji huyo hajatupia. Lakini Nabi akasisitiza wachezaji wote wakirejea mazoezini wataanzia na gym na watakiwasha kwelikweli.

Ki ambaye alisajiliwa kutoka ASEC Memosas ya Ivory Coast anasema jukumu lake ndani ya Yanga si kufunga tu bali ni maelekezo mengi anapewa na Kocha wake na wala hasikilizi kelele za nje ya uwanja.

“Nipo hapa kuipambania timu, ili icheze vizuri na kuwaweka wachezaji wenzangu kwenye nafasi nzuri ya kufanya vizuri, kama ntaweza kufunga nitafunga kwasababu ili uweze kufanya hivyo ni lazima uwe kwenye nafasi nzuri,” alisema na kuongeza;

“Kipaumbele changu cha kwanza ni kuifanya timu ishinde kutokana na mchezo ulivyo na nafurahi kuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu kupata matokeo kwenye mechi mbili mfululizo,” alisema mchezaji huyo ambaye tobo aliyompiga Tshabalala kwenye mechi ya watani bado ni gumzo mitandaoni.

Ki alisema anafurahi kucheza timu ambayo inatengeneza nafasi nyingi za kufunga na kufunga mabao ya ushindi na kuipa timu pointi kuhusu kufunga ni kazi yake muda ukifika atafanya hivyo japo sio muhimu sana kwake kama kuipa timu pointi.

Mchezaji huyo amecheza dakika 174 huku baadhi ya mashabiki wakiwemo wa Simba wakimkejeli mitandaoni kwanini hatupii kama Fiston Mayele.

Nabi amemzungumzia Ki kwamba ni mchezaji anayemtumia sehemu mbili tofauti kama winga ama kiungo mshambuliaji kulingana na mchezo unavyokuwa na wala hana presha nae.

“Nataka awatengenezee wachezaji wengine nafasi za kufunga, ndani ya michezo miwili aliyocheza nimeona uwezo wake wa kuisaidia timu ingawa bado nasisitiza natengeneza kikosi,” alisema.

KI katika dakika alizocheza kwenye mechi mbili akianza dhidi ya Polisi Tanzania ambapo alicheza dakika zote 90 na kuhusika kwenye kutengeneza bao la kusawazisha kwa kutoa pasi ya bao la Fiston Mayele na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Na mchezo wa pili dhidi ya Coastal Union alitumika kwa kucheza dakika 84 huku akipiga kona iliyozaa bao baada ya kuchonga mpira uliotua kwa beki Djuma Shaban ambaye alipiga mpira kwa kichwa na kumkuta Fiston Mayele aliyeunganisha mpira kwa kichwa na kutikisa nyavu.

SOMA NA HII  AHMED ALLY :- YANGA WANANYANYASA WACHEZAJI WAO...WANAHELA ZA KULIPA WASANII TU...

ASEC ALIKUWAJE

Kwa mujibu wa takwimu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, msimu uliomalizika, Aziz KI ameichezea mechi 29 kati ya 38 zilizoipa taji lao la 28 la Ligi Kuu ya kwao.

Katika mechi hizo amefunga mabao 10 na kuasisti sita, akiwa ametumia jumla ya dakika ya 2234 akipiga pasi 1074, huku akikokota mpira mara 87, kitu kilichomfanya rafiki na raia mwenzake anayepishana naye Yanga, Yacouba Sogne kushindwa kujizuia na kumsifia vilivyo.

Rekodi zinaonyesha pia kwenye mechi za kimataifa katika mechi 10 za Kombe la Shirikisho Afrika alitupia nyavuni mara nne.

Aziz KI amejiunga na Yanga dirisha hili la usajili kwa mkataba wa miaka miwili anaungana na Bernard Morrison ambaye tayari ametupia bao moja, Lazarous Kambole, Gael Bigirimana na Joyce Lomalisa ambao wote kwa pamoja wamesajiliwa katika dirisha linalofungwa Agosti 31.