Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSHINDA MECHI MBILI MFULULIZO..NABI ASHTUKIA JAMBO YANGA…APIGA MARUFUKU SOKA LA...

PAMOJA NA KUSHINDA MECHI MBILI MFULULIZO..NABI ASHTUKIA JAMBO YANGA…APIGA MARUFUKU SOKA LA SIMBA ….


Kuna soka flani la mipasi wachezaji wa Yanga wamelianzisha kwenye dakika za refa na wakati mwingine wanapoongoza bao mbili.

Mipasi hiyo imeonekana kuchochewa zaidi na mashabiki inapofika muda wa refa, lakini Kocha Nasreddine Nabi ameshtuka na kuchimba mkwara mzito.

Katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania Yanga ikifungua pazia la Ligi Kuu Bara, timu hiyo ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1, wachezaji hao walianza kugongeana pasi kuanzia dakika ya 89 walipigiana pasi zaidi ya 90 mpaka mpira ulipomalizika bila wapinzani kuugusa katoka dakika tatu za nyongeza.

Nabi amegundua kuna wakati wanacheza pasi nyingi ambazo zinawachelewesha kupata mabao mengi na amewataka wachezaji kubadilisha mara moja na kucheza pasi zinazolenga kupata mabao mengi kuliko kuridhika na mawili au matatu. Kocha huyo ambaye kwenye mechi na Coastal Union alionekana kutumia ishara za kurusha mikono akiwakemea wachezaji wapunguze mbwembwe, amesema kuwa ingawa falsafa ya soka lao ni kucheza kwa pasi lakini anataka pasi zinazofika katika lango la wapinzani ili wazalishe mabao ya kutosha na Yanga iogopwe.

“Sisemi kwamba wasipasiane kwa kuwa hii ni falsafa yetu hapa kwamba lazima tuuchezee mpira, lakini tunataka tuuchezee kwa kufika eneo la hatari la wapinzani tufunge mabao,” alisema Nabi ambaye ameweka rekodi ya kutopoteza mechi ya ligi mpaka sasa.

“Timu inatakiwa kupata mabao ya kutosha ambayo yataisaidia na pia yatawasaidia wao kama wachezaji kwenye takwimu zao lakini sio pasi nyingi sana bila kupata mabao ya kutosha.

“Tunatakiwa kufika eneo la hatari la wapinzani tutengeneze nafasi na tuzitumie nimewaambia hiki ndio ninachokitaka na sio vinginevyo,tunatakiwa kuimarika katika kufunga zaidi,” alisema Nabi ambaye ana uraia wa Ubelgiji na Tunisia.

Yanga imecheza mechi mbili za kwanza wakivuna pointi sita na mabao manne huku wakiruhusu bao moja katika ushindi dhidi ya Polisi Tanzania, kabla ya kuwafunga tena Coastal Union ya Tanga kwa mabao 2-0.

Nabi alisema nidhamu ya kusaka mabao ndio kitu ambacho pia kitawasaidia katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo yataanza mapema mwezi ujao wakifungua pazia dhidi ya Zalan na Sudan Kusini.

SOMA NA HII  ZAWAD MAUYA AUNGANA NA MSAFARA WA STARS BENIN

“Unapoingia katika mashindano ya Afrika unatakiwa kuwa na ulinzi mzuri lakini uwe na ubora wa kufunga mabao ya kutosha, hii ni nidhamu ambayo tunatakiwa kuanza kuijenga na sio kuangalia aina ya hizi mechi za ligi tunazocheza sasa.

“Usipokuwa na ubora wa kutumia nafasi unajiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele,najua mashabiki wanafurahia hizi pasi ni jambo zuri kwa kuwa nilisema wakati nafika hapa siku ya kwanza timu inatakiwa kushinda mataji na kuwafurahisha mashabiki kwa mpira mzuri tunaweza kushinda mabao mengi kisha tukawafurahisha mashabiki kwa pasi kama hizo.”

WASUDANI DAR

Zalan ya Sudan Kusini imewasilisha ombi mechi zao zote dhidi ya Mabingwa wa Tanzania, Yanga zichezwe hapa nchini Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Rais wa Yanga, Hersi Said amethibitisha kwamba wameshamalizana na Zalan katika maombi yao wakiuhamishia mchezo wa kwanza baina yao kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Wenzetu wamewasilisha maombi hayo kweli na sisi tukishirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) tumeshawakubalia na sasa taratibu zaidi zinaendelea,” alisema Hersi.

Zalan ilitakiwa kuanzia nyumbani kati ya Septemba 9-11,2022 mchezo ambao sasa utapigwa hapa nchini kisha timu hizo kurudiana tena baada ya wiki moja hapohapo Uwanja Mkapa.