Home Habari za michezo MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA JULIO NA NAMUNGO YAKE…AUKATAA UBINGWA YA YANGA….ADAI...

MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU KWA JULIO NA NAMUNGO YAKE…AUKATAA UBINGWA YA YANGA….ADAI BINGWA NI SIMBA…


Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo nyumbani, kocha msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo amekiri nafasi ya wao kumaliza ndani ya nne bora inazidi kufifia.

Namungo jana ilichapwa bao 1-0 na Coastal Union kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Lindi na kabla ya hapo ilipokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Polisi Tanzania.

Julio amesema wachezaji wake hawakuwa watulivu katika mchezo dhidi ya Coastal  Union licha ya kupata nafasi nyingi lakini akasema ndio soka lilivyo kwani hakuna mtu aliyepangiwa kushinda kila mechi.

“Tukubali ndio mpira ulivyo kwani siku nyingine mbona tunawafunga watu mabao matatu lakini wakati mwingine ndio matokeo huwa kuna siku unashinda na kuna wakati unapoteza”.  amesema Julio na kuongeza;

“Lengo letu ni kumaliza ligi katika nafasi ya tatu au nne lakini kwa matokeo haya nafikiri sasa nafasi  inazidi kuwa finyu lakini tutaendelea kupambana katika mechi mbili zilizobaki na mwisho tutajua tuko nafasi gani”.

Katika hatua nyingine, Julio amepinga Yanga SC kuwa mabingwa wapya wa NBC Premier league msimu huu akisema kuwa bingwa halisi atapatikana mpaka mwisho wa ligi ufike.

Julio ambaye ni mzuri wa kuongea maneno mengi harakaharaka , alisema kuwa anatofautiana na watu wanaosema Yanga bingwa kwani kwa ligi hii Simba bado ni bingwa endapo ikatoea Ligi Kuu ikasimamishwa na Rais wa Nchi.

“Mimi natofautiana na wanaosema Yanga Bingwa, kwa upande wangu mimi bado Simba ni Bingwa hadi mpaka pale kipenga cha mwisho cha msimu huu kitakapopulizwa ndio nitakubali kuwa Yanga ni mabingwa wapya, maana inawezekana wakati wowote ule Rias wa nchi akasimamisha ligi, na ikitokea hivyo kimantiki Simba ataendelea na ubingwa wake” alisema julio akihojiwa na Azam TV.

Namungo imebakiwa  mechi mbili zote za ugenini dhidi ya Mtibwa itakayofanyika Juni 26 kwenye uwanja wa Manungu Turiani na dhidi ya Mbeya City utakaofanyika Juni 29 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Timu hiyo ina ponti 37 ikiwa nafasi ya tano  sawa na Coastal yenye pointi 37 pia ikiwa nafasi ya sita wakati Azam yenye pointi 40 iko nafasi ya nne na Geita Gold ikiwa ya tatu na pointi 42.

SOMA NA HII  UONGOZI WAWATULIZA WANASIMBA, MRATIBU ATOA KAULI HII