Home Habari za michezo BAADA YA KUAMBULIA ZA USO KOMBE LA DUNIA…WABRAZIL WAMTAKA GUARDIOLA…

BAADA YA KUAMBULIA ZA USO KOMBE LA DUNIA…WABRAZIL WAMTAKA GUARDIOLA…

SHIRIKISHO la soka Brazil (CBF) itawasiliana na Pep Guardiola kwa ajili ya kumshawishi Mhispania huyo achukue mikoba ya Adenor Leonardo Bacchi, maarufu Tite kwa mujibu wa ripoti.

Brazil inasaka kocha mpya atakayeziba pengo la Tite baada ya kuondolewa kwenye robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia dhidi yab Croatia wiki iliyopita.

Brazil iliondoshwa baada ya Rodrygo na Marquinhos kukosa penalti Croatia wakiibuka vinara na kutinga nusu fainali ambayo watacheza dhidi ya Argentina leo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na jarida ka SPORT, Brazil inataka kumng’oa Guardiola licha ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukisuka kikosi cha Man City hadi mwaka 2025.

Rais wa shirikisho la Brazil, Ednaldo Rodrigues anayedili na masuala ya kuteua makocha, ataelewa kama Guardiola atagoma kuchukua mikoba ya Tite mwishoni mwa msimu wa 2022-20223 kwani mkataba wa Man City umembana kwasasa.

Aidha Guardiola ndio chaguo namba moja anayependekezwa kuziba nafasi ya Tite kwani shirikisho la Brazil inatambua kocha huyo ana kiwango bora cha dunia kwasasa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...ZAHERA AMNYOOSHEA KIDOLE MAYELE...AFUNGUKA SIMBA WALIVYO...