Home Habari za michezo WAFAHAMU WAPINZANI WA YANGA CAF…TIMU KIBONDE KWENYE KUNDI LAO HAWA HAPA…

WAFAHAMU WAPINZANI WA YANGA CAF…TIMU KIBONDE KWENYE KUNDI LAO HAWA HAPA…

Tetesi za Usajili Yanga

HATIMAYE Yanga imewajua wapinzani wake watatu watakaokutana nao katika mechi sita za Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika droo iliyofanyika leo jijini Cairo ikiendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Yanga imepangwa kundi D sambamba na timu za TP Mazembe kutoka DR Congo,Real Bamako ya Mali na US Monastir ya Tunisia lakini ndani ya timu hizo kuna koneksheni tatu ambazo Yanga itazitumia kunasa taarifa muhimu za wapinzani wao.

Yanga itakapokutana na Mazembe itakuwa na akili mbili zitakazowanufaisha wa kwanza ni Afisa Mtendaji wao Mkuu Andre Mtine ambaye ametua hapo akitokea kwa wakongomani hao.

Mtine amefanya kazi Mazembe kabla ya kutua Yanga akiwa mtu muhimu pembeni ya tajiri wa Wakongomani hao Moise Katumbi kuna nafasi kubwa ya Mtine kuinufaisha Yanga katika kujua mambo mengi ya ndani ya klabu hiyo.

Ukiachana na Mtine Yanga pia ina wachezaji wanne raia wa Congo ambao wanaijua vyema Mazembe ambao ni mabeki Joyce Lomalisa, Yannick Bangala,Djuma Shaban, Jesus Moloko,Fiston Mayele na Heritier Makambo.

Ingawa mastaa wote hao hawajawahi kuitumikia Mazembe kwa undani lakini shuti wanajua taarifa nyingi za klabu hiyo kwa kuwa walikuwa watani wao wazito.

Ndani ya Mazembe pia kuna faida moja kwao uwepo wa kiungo wao zamani Mukoko Tonombe ambaye alisajiliwa hapo akitokea Yanga msimu uliopita ingawa amekuwa hapati nafasi ya kutosha ndani ya kikosi hicho.

US Monastir

Klabu pinzani ya Club Africain iliyowapa tiketi Yanga kutinga hatua ya makundi kutoka ardhi ya Tunisia.

Yanga hapa pia ina watu watatu wazito ambao watainufaisha klabu hiyo katika kujua taarifa za msingi za wapinzani wao ambao ni kocha mkuu Nasreddine Nabi, kocha wa viungo Helmy Gueldich na daktari wa viungo Yousef Mohamed ambaye anatoka katika mji unaotoka klabu hiyo.

Real Bamako
Klabu kutoka nchini Mali ambayo ipo na Yanga kundi moja hapa maana halisi kwamba kipa wao Djigui Diarra anarudi nyumbani.

Diara anawajua vyema Real Bamako kwa kuwa alikuwa anacheza ligi hiyo ya Mali akiitumikia klabu bingwa Stade Mallien ya huko ambapo hapo atakuwa mchora ramani kwa klabu yake watakapokutana.

SOMA NA HII  WAZIRI NDUMBARO AMPA ZAWADI NYOTA WA CRYSTAL PALACE, AAHIDI KUWALETA MASTAA BONGO