Home Habari za michezo YANGA WASHINDWE WENYEWE AISEE…CAF WAIPA URAHISI WA KUBEBA UBINGWA WA SHIRIKISHO…

YANGA WASHINDWE WENYEWE AISEE…CAF WAIPA URAHISI WA KUBEBA UBINGWA WA SHIRIKISHO…

Habari za Yanga SC

Kuanzia msimu huu wa mashindano ya CAF, mechi za fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika zimerejeshwa katika mtindo wa nyumbani na ugenini.

Kwa misimu kadhaa iliyopita, mechi za fainali zilipigwa katika uwanja huru unaopendekezwa kufuata vigezo walivyojiwekea CAF.

Hata hivyo baada ya fainali kati ya Al Ahly dhidi ya Wydad iliyopigwa Morocco na Al Ahly kuwasilisha malalamiko yao CAF kupinga mechi ya fainali kupigwa katika moja ya klabu iliyotinga fainali, utaratibu umebadilishwa tena na kurejeshwa kama zamani.

Kama Yanga itatinga fainali, itakuwa na mechi mbili za kusaka ubingwa wa Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas au USM Alger.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA SHIRIKISHO CAF...WASAUZI WAANZA SONGOMBINGO...WAUOGOPA UWANJA WA MKAPA ETI...