Home Uncategorized MSHAMBULIAJI HUYU WA BURUNDI AKUBALI KUVAA UZI WA YANGA

MSHAMBULIAJI HUYU WA BURUNDI AKUBALI KUVAA UZI WA YANGA


BIGIRIMANA Blaise, raia wa Burundi anayekipiga ndani ya Namungo FC amesema kuwa hana hiyana ya kutua ndani ya Klabu ya Yanga iwapo watafuata taratibu za usajili.

Blaise kabla ya msimu kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona alikuwa kwenye mwendo mzuri wa kucheka na nyavu ambapo alikuwa ametupia mabao 10 kati ya 34 yalifungwa na klabu yake.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Blaise alisema kuwa awali kulikuwa na viongozi wa Yanga waliwahi kumfuata ili wapate saini yake ila walighairi baada ya kuona ameshatua Namungo.
“Kabla ya kutua Namungo wakati nipo Stand United niliwahi kuzungumza na viongozi wa Yanga na tulikuwa kwenye hatua nzuri ila kuna mambo hayakuenda sawa nikaibukia Namungo, kwa sasa nimekuwa nikiskia kama wananihitaji tena hilo siwezi kuzungumza kwa sasa.
“Bado nina mkataba na Namungo ambao utaisha pindi msimu ukiisha iwapo watakuja na tukafikiana makubaliano sina hiyana nipo tayari kuvaa jezi ya Yanga, sichagui hata ikitokea ni Kagera Sugar ama Simba kikubwa maelewano na utaratibu ufuatwe,” amesema.
SOMA NA HII  MAISHA MAPYA NDANI YA TIMU MPYA ILA URAFIKI WAO KITAMBO UNAENDELEA