Home Uncategorized YANGA YAPIGWA BAO NA SIMBA KWA MTUPIAJI HUYU

YANGA YAPIGWA BAO NA SIMBA KWA MTUPIAJI HUYU

INAELEZWA kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye rada za kuiwinda saini ya Heritier Makambo aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo. 

Makambo aliachana na Yanga msimu wa 2017/18 akiwa ni namba tatu kwa kutupia ambapo wa kwanza alikuwa ni Meddie Kagere wa Simba aliyetupia 23 na Salim Aiyee aliyekuwa Mwadui FC alitupia 18.

Kwa sasa Makambo anakipiga ndani ya Klabu ya Horoya AC ya nchini Guinea alisaini dili la miaka mitatu kuitumikia timu hiyo. 

Habari zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Simba umeshaanza kufanya mazungumzo na mabosi wa Horoya ili kupata saini ya nyota huyo mwenye uzoefu wa kucheka na nyavu.

“Msimu ujao Yanga itapata tabu kwani idadi kubwa ya wachezaji wao wanaweza kuonekana wakikipiga ndani ya Simba na mpaka sasa asilimia kubwa kwa Makambo kukipiga Simba msimu ujao.

“Yanga ilishindwa kuvunja mkataba wake kule Horoya AC ila ndani ya Simba kila kitu kimekuwa sawa na bodi imekubali kuingia chimbo kuiwinda saini yake,” ilieleza taarifa hiyo. 

Awali taarifa zilieleza kuwa Yanga ilikuwa inaiwinda saini ya nyota huyo ili arejee ndani ya kikosi hicho.

SOMA NA HII  MSUVA AWAZIDI KETE WACHEZAJI WOTE EL JADIDA