Home Uncategorized GIROUD AKUBALI KUTUA INTER MILAN MSIMU UJAO

GIROUD AKUBALI KUTUA INTER MILAN MSIMU UJAO

Paris, Ufaransa. Olivier Giroud amefikia mwafaka kuhusiana na masilahi binafsi na Inter Milan inayotaka huduma katika majira ya kiangazi.

Taarifa za awali zimedai mshambuliaji nguli wa Chelsea atatua  San Siro kwa mkataba wa miaka miwili.

Conte aliwahi kumtupia ndoano Mfaransa huyo katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwaka huu.

Mshambuliaji huyo nguli huyo anasaka timu baada ya kupokwa namba na kinda Tammy Abraham.

Tammy anaonekana kuwa chaguo la kwanza kwa kocha Frank Lampard. Inter Milan inaweza kupata saini ya Giroud akiwa mchezaji huru majira ya kiangazi msimu ujao.

Lazio imekuwa ikifuatilia nyendo za Giroud aliyeipa ubingwa wa dunia Ufaransa katika fainali za mwaka jana.

Giroud analipwa mshahara wa Pauni135,000 lakini amekuwa kupunguza hadi Pauni110,000 kwa wiki fedha ambazo idadi kubwa ya klabu Italia zinawalipa wachezaji wake.

SOMA NA HII  NIYONZIMA APEWA SOMO NA SAMAKIBA