Home Uncategorized MAISHA MAPYA NDANI YA TIMU MPYA ILA URAFIKI WAO KITAMBO UNAENDELEA

MAISHA MAPYA NDANI YA TIMU MPYA ILA URAFIKI WAO KITAMBO UNAENDELEA

 

HAWA ni marafiki wa kitambo sasa wanaendelea kuwa marafiki ndani ya timu zao mpya namna hii:-

Awesu Awesu v David Kissu 

Wote wapo zao Azam FC. Walikipiga pamoja Singida United msimu wa 2008/19, Kisu msimu uliopita alikuwa  Gor Mahia na Awesu alikuwa Kagera Sugar sasa wote wapo Azam FC.

Joash Onyango v Francis Kahata 

Wote ni raia wa Kenya, Kahata na Onyango ni washakji kutoka ndani ya timu ya Taifa ya Kenya, ‘Harambee Stars’ alianza kuibuka Kahata msimu wa 2019/20 kisha Onyango kamfuata mshikaji wake ndani ya Simba 2020/21.

Kapama, Materema na Ufudu

Nyota hawa walikuwa washkaji ndani ya JKT Tanzania msimu wa 2018/19,  msimu wa 2019/20 wakatengana Materema alibaki JKT Tanzania,  Ally Nassor,’Ufudu’ aliibukia Mbeya City na Nassor Kapama akaibukia Kagera Sugar ila sasa wote wapo Kagera Sugar 

Bwalya v Chama

Ni washakji kutoka timu ya Taifa ya Zambia,’ Chipolopolo’ sasa wote wawili, Larry Bwalya na Clatous Chama wanaendeleza urafiki ndani ya Simba msimu wa 2020/21.

Kalambo na Peter Mapunda 

Aron Kalambo na Mapunda walikuwa washkaji ndani ya Mbeya City na sasa wapo pamoja ndani ya Dodoma Jiji.

SOMA NA HII  YANGA WAMTAJA MCHEZAJI WA SIMBA KUWA NDIYE BORA NDANI YA LIGI KUU BARA