Home Uncategorized MAN UNITED YAJIPA MATUMAINI KWA SANCHO

MAN UNITED YAJIPA MATUMAINI KWA SANCHO

London, England. Manchester United imejipa matumaini ya kushinda vita ya kuwania saini ya Jadon Sancho.

Sancho ameteka vyombo vya habari Ulaya baada ya kuzivutia  idadi kubwa ya klab zinazotaka kumwa katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Man United ina matumaini kumpata Sancho baada ya kuteta na klabu yake ya Borussiaa Dortmund na mchezaji husika.

Klabu hiyo italazimika kufanya kazi ya ziada kupata saini yake kwa kuwa Dortmund imepanga kumuongeza dau la mshahara ili kumbakiza.

Thamani ya Sancho inadaiwa kufikia Pauni100 milioni katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Sancho amekuwa katika kiwango bora tangu alipotua katika Ligi Kuu Ujerumani akifunga mabao 17 na kutengeneza mengine 19 msimu huu.

SOMA NA HII  GWAMBINA YAPOTEZA POINTI TATU MBELE YA BIASHARA UNITED