Home Habari za michezo KMC FC YAFUTA NYAYO ZA SIMBA NA YANGA…WATENGA BILIONI 1 YA KUSHUSHA...

KMC FC YAFUTA NYAYO ZA SIMBA NA YANGA…WATENGA BILIONI 1 YA KUSHUSHA VYUMA VYA KAZI..

Tetesi za Usajili Bongo

BAADA ya klabu ya KMC kujihakikishia kucheza Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao viongozi wa timu hiyo wametenga bajeti ya Sh1 bilioni ambazo zitatumika kwa ajili ya usajili wa mastaa wengine wapya.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa, baada ya kusuasua kwa msimu uliopita wameamua kuongeza kiasi hicho ili kutengeneza kikosi imara.

“Mkurugenzi wetu, Hanifa Suleiman Hamza hataki kuona timu ikipitia kile ilichopitia ndio maana bajeti imekuwa ni kubwa zaidi ya msimu uliopita ambao tulitenga Sh700 milioni,” alisema Mwagala.

Wakati bajeti hiyo ikitengwa inafahamika kuwa KMC imenasa saini ya Juma Shemvuni kutoka Mbeya City, Muhusin Malima (Dodoma Jiji), Rodgers Gabriel (Pamba) na Andrew Simchimba wa Ihefu.

11 WAPIGWA PANGA.

Katika hatua nyingine uongozi wa KMC FC umeamua kuachana na mastaa wao 11 ambao wataenda kutafuta changamoto mpya nje ya timu hiyo, huku ukianza kukisuka kikosi bora kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24.

Ikumbukwe kuwa KMC FC walibakia Ligi Kuu baada ya kushinda mechi zao za Play Off dhidi ya Mbeya City ambao wameangukia kwenye Ligi ya Championship, kufuatia kufungwa na Mashujaa FC ya Kigoma.

Afisa Habari wa KMC FC, Christina Mwagala amesema: “Ni kweli tumeachana na mastaa 11 kwa lengo la kusajili wachezaji wengine ambao mwalimu kapendekeza na wachezaji ambao tumeachana nao wote tumeshawapa barua zao, kila mchezaji anafahamu kuwa hatakuwepo msimu ujao.

“Wachezaji ambao tumewaacha ni Erick Manyama, Steve Nzigamasabo, Mohamed Samata, David Kisu Mapigano, Nurdin Balora, Isaac Kachwere, Ally Ramadhan ‘Oviedo’, Abdul Hillary, Frank Zakaria na Denis Richard.

“Tunawashukuru kwa mchango wao mkubwa wa msimu wa 2022/2023 ambao walitusaidia kupambana mpaka kubaki ligi kuu baada ya kucheza playoff na Mbeya City.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...AHMED ALLY AIBUKA NA JIPYA SIMBA...VUNJA BEI ATAJWA...