Home Habari za michezo BOCCO, MBRAZILI WAIPIGA BITI LA KUFA MTU AL AHLY ….

BOCCO, MBRAZILI WAIPIGA BITI LA KUFA MTU AL AHLY ….

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa hana presha yoyote kuelekea mchezo wa kesho wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly licha ya kukiri itakuwa mechi ngumu.

Robertinho amesema kuwa anaiheshimu Al Ahly kwakuwa ni timu kubwa na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini Simba pia ni kubwa na ipo tayari kwa mchezo wa kesho.

Robertinho ameongeza kuwa pamoja na ubora na uzoefu walionao Al Ahly barani Afrika lakini mpira ni sasa hivyo tupo tayari kwa dakika 90 za kesho kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

“Sina presha na mchezo wa kesho licha yakuwa ni mkubwa, hata mimi nikiwa mchezaji kule Brazil nimewahi kukutana na mechi kama hizi kwahiyo naifurahia na sina presha.”

“Ni kweli tunacheza mechi kubwa, Al Ahly ni timu bora na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mpira ni sasa na tupo tayari kwa dakika 90 za kesho,” amesema Robertinho.

Akizungumzia kuhusu kurejea kwa mlinzi wa kati, Henock Inonga ambaye alikuwa majeruhi Robertinho amesema “Henock ni mchezaji bora barani Afrika urejeo wake utatuongezea nguvu na nategemea kumtumia kwenye mchezo wa kesho.”

Kwa upande wake ,Nahodha wa timu, John Bocco amesema licha ya ugumu wa mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly lakini uwepo wa mashabiki ambao watakuja kwa wingi uwanjani utatuongezea nguvu.

Bocco amesema mashabiki wana mchango mkubwa kuisaidia timu kupata ushindi hivyo watatumia nafasi hiyo kuhakikisha wanashinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Bocco ameongeza kuwa haitakuwa mechi rahisi na kila mchezaji analijua hilo na maandalizi waliyopata anaamini watapata ushindi.

“Haitakuwa mechi rahisi, Al Ahly ni timu bora lakini nasi tuna timu nzuri, tuna faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao watakuwa wamezaja uwanja.”

“Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo na tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya ili tuwe sehemu salama katika mechi ya marudiano,” amesema Bocco.

SOMA NA HII  MATOLA:- KWA HALII....MHHH UBINGWA UTAKUWA MGUMU SIMBA....