Home Simba SC CLATOUS CHAMA AFUNGUKA ISHU YA TUZO BONGO

CLATOUS CHAMA AFUNGUKA ISHU YA TUZO BONGO

 CLATOUS Chama nyota wa Simba amesema kuwa anahitaji tuzo zake zote ambazo alisepa  nazo msimu uliopita kwa kuwa anastahili.

2019/20 kiungo huyo alisepa na tuzo tatu ndani ya Ligi Kuu Bara ya kwanza ilikuwa ni kiungo bora ya pili ni mchezaji bora na ya tatu ni kuwa ndani ya kikosi bora cha msimu.

Katika tuzo hizo ambazo hutolewa na Bodi ya Ligi Tanzania kwa kushirikiana na mdhamini mkuu ambaye ni Vodacom, Chama alikuwa amefunga mabao mawili na pasi 10 za mabao 

Hivyo alihusika katika mabao 12 kati ya 78 yaliyofungwa na timu hiyo zama za Sven Vandenbroec ambaye naye alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimi baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la ligi.

Msimu huu wa 2020/21 amehusika kwenye mabao 23, akifunga nane na pasi 15 za mabao kati ya 78 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyotwaa ubingwa.

Chama amesema:”Namba hazidanyi hivyo ikiwa utasema jambo kuhusu tuzo basi nastahili na nahitaji kupewa tuzo, tusubiri na tuone itakuaje,”.

SOMA NA HII  EEHE...UMESIKIA ALICHOSEMA MUGALU HUKO SIMBA..?...AFUNGUKA A-Z YALIYOJIFICHA MOYONI...