Home Geita Gold FC UBABE WA YANGA WAIHAMISHA GEITA GOLD

UBABE WA YANGA WAIHAMISHA GEITA GOLD

Habari za Yanga

Matokeo mabaya inayopata timu ya Geita Gold, yanadaiwa kuihamisha kutoka katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kwa mechi zitakazohusisha timu za Simba SC na Young Africans.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Habari wa timu hiyo, Samwel Dida wakati akizungumza jijini Mwanza amesema kuwa wana imani timu yao haina bahati na uwanja huo.

“Hatuko salama sana maana tuna alama nne katika michezo minne tuliyocheza ya Ligi Kuu, hivyo uongozi na dawati la ufundi tunarudi tumeteleza na kutafakari wapi kurekebisha makosa,”amesema

“Tunafikiria kubadilisha uwanja tuone kama kuna tofauti,tunaangalia uwanja wa Mwadui, wakati tukisubiri wetu ukamilike. Naamini uwanja tutafanya vizuri zaidi,”amesema.

Dida ameongeza kuwa uwanja wao huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 15,000 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 85.

SOMA NA HII  MAYELE NA MUSONDA WAMPA JEURI RAISI...YANGA ITAWEKA REKODI MSIMU HUU...TIMU IPO VIZURI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here