Home Habari za michezo BAADA YA KUONA UWEZO WA SAWADOGO…MGUNDA KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKAMTAJA NASSOR KAPAMA…

BAADA YA KUONA UWEZO WA SAWADOGO…MGUNDA KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKAMTAJA NASSOR KAPAMA…

Habari za Simba

Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amefichua kiungo, Ismail Sawadogo ni fundi na ni aina ya wachezaji aliokuwa akiwahitaji sana Msimbazi.

Mgunda ambaye ni Kocha wa zamani wa Coastal Union, alisema Sawadogo bado hajafikia ule utimamu wa mwili kama wanaouhitaji ila muda si mrefu, mashabiki na wanachama watamwelewa na kumpa heshima yake.

Alisema Sawadogo ni mmoja wa wachezaji wazuri aliyekuja kuongeza ushindani kwenye eneo la kiungo la Simba kulingana na wachezaji walio kwenye nafasi hiyo.

“Eneo la kiungo kama wote wakiwa fiti, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin, Sawadogo, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Nassoro Kapama unampanga nani na yupi wa kumuacha nje.

“Simba tulikuwa tunahitaji mchezaji wa aina yake ila bado hajapata muda wa kutosha kufanya mazoezi na wachezaji wenzake, kuzoea mazingira pamoja na ushindani wa ligi naamini anakwenda kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chetu,” alisema Mgunda ambaye amewahi kuwa kwenye benchi la Taifa Stars.

“Changamoto alipotokea hakuwa amepata muda wa kucheza mechi za kimashindano kwa hali hiyo hauwezi kupewa michezo yenye ushindani, mchezaji ukatumikia kwa kiwango cha juu moja kwa moja,” alisema Kocha huyo ambaye bosi wake Oliveira Robertinho amemhakikishia kibarua chake kiko salama.

“Kutokana na mazingira hayo lazima Sawadogo atafanya mazoezi mengi mbalimbali, naamini hata yake binafsi kwa ajili ya kurudisha na kutengeneza utimamu wa mwili ili kuonyesha kipaji na ubora wake zaidi ya ilivyokuwa kwenye michezo miwili iliyopita.

“Ukiangalia mechi na Dodoma Jiji hakuwa amepata muda wa kufanya mazoezi na timu kwa pamoja Sawadogo tumemtumia na amefanya vizuri kwenye eneo hilo licha ya kuwakosa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza.

“Mechi na Coastal ndani ya muda mfupi tu amekuwa msaada wa kuzuia mashambulizi, kuanzisha mashambulizi kutokana na hilo namwona tukiendelea kuwa nae kwenye mazoezi atakuja kuwa mchezaji imara na bora wa kigeni nchini.”

Sawadogo ameitumikia Simba kwenye mechi mbili za kimashindano zote akianza kikosi cha kwanza dhidi ya Dodoma Jiji na Coastal Union zote timu yake ikipata ushindi wa bao 1-0.

Katika hatua nyingine kikosi cha Simba kilifanya mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena kisha kuingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya mchezo wa dhidi ya Singida Big Stars.

Baada ya mechi ya Singida Simba itakwenda ugenini kuvaa na Horoya Februari 11 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kuwavaa Raja Casablanca nyumbani. Kwenye mazoezi ya leo Jumatano jioni kocha mkuu, Oliveira Robertinho aliyekosekana kwa muda wa wiki moja atakuwepo.

SOMA NA HII  ZA NDANIII KABISA....BAADA YA MORRISON KUPIGWA CHINI....MOSES PHIRI IMEBAKI TIKETI YA NDEGE TU ATUA ZAKE BONGO...